Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya yatakiwa kutekeleza mifumo ya haki ili kukaribisha duru la maridhiano

Libya yatakiwa kutekeleza mifumo ya haki ili kukaribisha duru la maridhiano

Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imeitala Libya kuanza kutekeleza kwa vitendo mpango mkakati wenye sura ya kuleta haki na usawa ili kufanikisha duru la maridhiano kwa ajili ya kuponyesha majeraha yaliyoibuliwa wakati wa vita vya kikabili vilivyoishia kuundosha utawala wa kidikiteta wa Muamary Gafaf.

Duru hilo la maridhiano limepangwa kuanza mwaka kesho likileng a kuleta suluhu ya pamoja na kuzika hali ya kuhasimiana iliyofufuka wakati wa vugu vugu la kuupinga utawala wa Gadafi.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo katika ripoti yake umesema kuwa kuanzishwa kwa duru la mpito la uletaji haki ndiyo karata muhimu itayosaidia kustawisha kwa taifa hilo.

Taifa hilo la Libya kwa hivi sasa liko kwenye kipindi cha mpito kuelekea kwenye ujenzi kuelekea kwenye misingi ya kidemokrasia baada ya kupita miongo kadhaa ya utawala wa kidikteta wa Muammar al-Qadhafi.