Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka Sahel Magharibi iungwe mkono kukabili changamoto

UM wataka Sahel Magharibi iungwe mkono kukabili changamoto

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa amelitolea mwito Baraza la Usalama pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla kuunga mkono mpango wenye shabaha ya kutanzua mikwamo inayoendelea kulikumba eneo la Sahel ambalo pia linaandamwana mzozo wa kisiasa.

Jeffrey Feltman amewaambia wajumbe wa baraza hilo kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kuziunga mkono juhudi zinazoendelea kuchukuliwa wakati huo ambazo zimelenga kufufua matumaini ya utulivu na wakati huo huo kuzipatia majibu changamoto zinazojitokeza.

Amesema ni muhimu kutambua kuwa ustawi bora kwa taifa hilo haitegemei tu kuungwa mkono kisiasa, lakini kuna uwanja mpana zaidi ambao unapaswa kutupiwa macho ikiwemo maeneo ya ikiwemo ameneo ya misaada ya kiutu.

Sahal iliyoko Afrika Magharibi inaandamwa mchanganyiko wa matatizo ikiwemo ukosefu wa mfumo dhabiti wa kikatibu ambao umezorotesha pia hali ya kisiasa. Pia eneo hilo linaandamwa na makundi ya waasi yanayochochea ukosefu wa amani.