Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi wa zamani wa Somalia ashinda tuzo ya UNHCR

Mkimbizi wa zamani wa Somalia ashinda tuzo ya UNHCR

Mkimbizi wa zamani kutoka Somalia ndiye mshindi wa tuzo la mwaka huu la Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR.

Shirika la UNHCR limetangaza leo kuwa Hawa Aden Mohamed ndiye mshindi wa tuzo ya wakimbizi ya Nansen ya mwaka 2012.

Bi Hawa Mohamed ni mwanzilishi wa kituo cha elimu cha Galkayo Education Centre for Peace and Development katika jimbo la Puntland, kaskazini mashariki mwa Somalia.

Bi Mohamed alirudi Somalia mnamo mwaka 1995, na kuanzisha mpango wa elimu kwa ajili ya kuwasaidia watu walolazimika kuhama makwao kwa sababu ya migogoro na ukame nchini Somalia. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)