Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Warsha ya kutoa mafunzo kuhusu usimamizi wa kambi kuanza rasmi kesho Namibia

Warsha ya kutoa mafunzo kuhusu usimamizi wa kambi kuanza rasmi kesho Namibia

Warsha ya siku mbili ambayo inatarajiwa kuwapa mafunzo wafanyikazi wa serikali nchini Namibia na wa shirika la msalaba mwekundu nchini Namibia kuhusu usimamizi wa kambi itang’oa nanga hapo kesho mjini Windhoek nchini Namibia. Warsha hiyo inayofadhiliwa na jumuiya ya Ulaya na kuandaliwa kwa ushirikino na shirika la kimataifa la uhamijaji IOM inalenga kutoa mafunzo kuhusu usimamizi wa kambi kusaidia maeneo saba yanayokumwa na majanga ya mara kwa mara ya Caprivi, Kavango, Kunene, Ohangwena, Omusati, Oshana na Oshikoto kaskazini na kaskazini mashariki mwa nchi. IOM iliiomba ofisi ya Waziri mkuu kuandaa warsha hiyo baada ya kutokea mafuriko mabaya yaliyoikumba nchi hiyo mwaka 2011 hadi kusababisha watu kuhama.

Namibia pia huwa inakabiliwa na majanga ya ukame. Kati ya washiriki watakuwa ni watoa mafunzo waliohitimo ambao watajadili changamoto na fursa zilizopo na kupanga njia za kutoa mafunzo kuhusu majanga kwa watoa huduma kwenye sehemu zinazokumbwa zaidi na majanga.