Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rekodi ya miaka 90 ya viwango vya joto Libya ilikuwa na dosari:WMO

Rekodi ya miaka 90 ya viwango vya joto Libya ilikuwa na dosari:WMO

Jopo la Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limesema kuwa rekodi ya miaka 90 kufikia leo, iliyoshikiliwa na eneo la El Azizia nchini Libya kama mahali penye viwango vya juu zaidi vya joto duniani ni potovu, kwa sababu ya dosari katika kurekodi viwango hivyo vya joto.

Tangazo hilo linafuatia utafiti wa tahadhari uliofanywa wakati wa mapigano ya mapinduzi nchini Libya mwaka 2011. Mbuga ya kitaifa ya Death Valley katika jimbo la California, Marekani, ndipo sasa mahali rasmi penye viwango vya juu zaidi vya joto ulimwenguni.

Rekodi hii ni yenye umuhimu kwa watabiri wa hali ya hewa, kama mlima Everest ulivyo kwa wanajiografia. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)