Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zazuia mazungumzo ya amani Syria: Ban

Ghasia zazuia mazungumzo ya amani Syria: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelaani matumizi ya nguvu za kijeshi yanayoendelea kutekelezwa na vikosi vya serikali ya Syria na vile vya waasi. Bwana Ban amesema kushindwa kufanya mazungumzo kunafanya juhudi za Umoja wa Mataifa kuwezesha kuundwa serikali ya mpito na kuendeleza amani ambayo watu wa Syria wanahitaji.

Akilihutubia Baraza la Haki za Binadam la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Bwana Ban amesema wanaotekeleza uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Syria ni lazima wakabiliwe na mkono wa sheria, bila kujali wanaegemea upande upi.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Katibu Mkuu pia ameelezea kusikitishwa kwake na ukiukaji mkubwa wa haki za binadam dhidi ya watu wa kaskazini mwa Mali, na kutoa wito kwa Baraza la Haki za Binadamu kukabiliana nao ipasavyo.