Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa Syria unachochewa zaidi na silaha:Pillay

Mzozo wa Syria unachochewa zaidi na silaha:Pillay

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi pillay amesema kuwa kuwauzia risasi wanajeshi ya Syria pamoja na vikosi vya upinzani sio suluhu la mzozo ulio nchini Syria. Akihutubia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Pillay amesema kuwa kuendelea kuzorota kwa usalama kunawazuia watoa huduma za kibinadamu wanaowahudumia raia milioni 2.5 walioathiriwa na mzozo. Amesema kuwa ukiukaji wa haki za binadamu unaoweza kutajwa kuwa uhalifu wa kivita umeripotiwa kutoka pande zote mbili.

Ameongeza kuwa mashambulizi ya mabomu kwenye sehemu zenye watu wengi na vikosi vya serikali , mauaji yasiyofuata sheria na dhuluma kutoka kwa makundi ya waasi huenda vikaorodheshwa kuwa uhalifu wa kivita.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)