Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 20 ya Mkataba wa UNECE kuhusu Maji

Miaka 20 ya Mkataba wa UNECE kuhusu Maji

Mkataba kuhusu udhibiti na matumizi ya vianzo vya maji vinavyovuka mipaka ya kimataifa ulitiwa saini mwaka 1992 katika mji wa Helsinki. Ili kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo, serikali ya Finland imeandaa mkutano kati ya tahere 3 na 4 Septemba 2012.

Katika mkutano huo, washirika wamejadili hatua zilizopigwa katika miongo miwili iliyopita, pamoja na mitazamo ya siku zijazo ya mkataba huo, pamoja na kwamba unahitajika kufanywa mkataba wa ulimwengu mzima, huku ikitarajiwa utafanyiwa marekebisho ili uhusishe Umoja wa Mataifa na mataifa mengine nje ya Tume ya Kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ulaya, UNECE.

Mkataba huo unatoa mwongozo wa kubadilishana uzoefu na ujuzi katika kukabiliana na pengo lililopo kati ya matumizi ya maji na upatikanaji wa maji hayo, kuzorota kwa viwango vya ubora wa maji, mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na uhusiano uliopo kati ya maji, chakula na nishati katika maeneo ya mipakani.