Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya Gambia yanarudisha nyuma juhudi za kulinda haki za binadamu: Pillay

Mauaji ya Gambia yanarudisha nyuma juhudi za kulinda haki za binadamu: Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema kuwa amesikitishwa sana kuwa baada ya miaka 27 bila kutekeleza rasmi hukumu ya kunyonga nchini Gambia, wafungwa tisa walohukumiwa kifo waliuawa wiki hii kwa kufyatuliwa risasi katika tukio lililoonyesha kupiga hatua nyuma katika ulinzi wa haki za binadamu nchini humo.

Bi Pillay amesema kwa takriban miongo mitatu, Gambia imekuwa mojawepo ya idadi inayoongezeka ya mataifa yasiyotekeleza hukumu ya kifo, hadi tukio hili la ghafla na la kuhuzunisha lililobadili mkondo. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)