Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaitaka Bangladesh kuondoa marufuku kwa mashirika yasiyokuwa ya serikali

UNHCR yaitaka Bangladesh kuondoa marufuku kwa mashirika yasiyokuwa ya serikali

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linatoa wito kwa serikali ya Bangladesh kuhakikisha kuwa misaada kutoka kwa mashirika yasiyokuwa ya seriali imeendea kutolewa kwa watu ambao hawajasajiliwa kutoka jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Juma lililopita mashirika yasiyokuwa ya serikali yakiwemo la Medecins Sans Frontières, Action Contre La Faim and Muslim Aid UK yaliamrishwa na serikali ya Bangladesh kusitisha shughuli zao kwenye kambi ambazo hazijasajiliwa kusini mashariki mwa nchi. UNHCR inasema kuwa ikiwa agizo hilo litatekelezwa litakuwa lenye athari kubwa kwa karibu watu 40,000 ambao hawajasajiliwa walioikimbia Myanmar miaka ya hivi karibuni. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)