Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada zaidi inahitajika kuwafadhili wakimbizi wa Mali walioko mafichoni:Guterres

Misaada zaidi inahitajika kuwafadhili wakimbizi wa Mali walioko mafichoni:Guterres

Kamishna Mkuu wa shirika la kuwahumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR António Guterres amesema kuwa wakati huu kuna hali ya mkwamo inayowandama mamia ya wakimbizi wa Mali waliokwama vichakana na akaenda mbali zaidi kwa kuitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza mafunga ya msaada kwa ajili ya kuwanusuru raia hao.

Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuogeza misaada zaidi ili kufanikisha operesheni za kuwafikishia misaada ya dhararu hasa kutokana na maeneo wanakopatikana.

Akiwa katika ziara ya siku tatu katika nchi jirani ya Burkina Faso nchi ambayo inahifadhi kiasi cha wakimbizi 107,000 wa Mali, Kamishna huyo amesema kuwa wakati idadi ya wakimbizi wakizidi kuongezeka kwenye eneo hilo, ndivyo hali ngumu na mateso inavyowandama raia hao.

Kiasi hicho cha wakimbizi kinachohifadhiwa nchini Burkina Faso ni kikubwa zaidi kwa wakati huo katika eneo hilo.Maeflu ya watu wanaendelea kuyahama maeneo yao na kutorokea maeneo ya jirani kutokana na kuzidi kushadidi kwa machafuo baina ya vikosi vya serikali na majeshi y