Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi Hafifu Zinazuia Utendaji wa Haki Kyrgyzstan:Pillay

Taasisi Hafifu Zinazuia Utendaji wa Haki Kyrgyzstan:Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, amesema kuwa kutokuwepo taasisi thabiti kunaendelea kuwa kizuizi katika kutekeleza haki na uongozi wa kisheria nhcini Kyrgyzstan.

Bi Pillay amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Bishek, wakati wa ziara yake nchini humo. Amesema serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa kuna uajibikaji kwa ajili ya uhalifu na ukiukaji wa haki za binadamu, ukiwemo ule unaofanywa na serikali, ili kuhakikisha haki inatendeka kwa waathirika na jamaa zao.

Akikutana na rais wa nchi hiyo, Bi Pillay ameipongeza serikali yake kwa kusema kuwa imejitolea kukabiliana na ufisadi, ambao ni tatizo kubwa katika mataifa ya kanda nzima, ikiwemo Kyrgyzstan.