Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU na Uturuki lazima watoe Kipaumbele Kwa Haki za Binadamu:UM

EU na Uturuki lazima watoe Kipaumbele Kwa Haki za Binadamu:UM

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wahamiaji, François Crépeau, ametoa wito kwa Uturuki na Muungano wa Ulaya kutoa kipaumbele kwa haki za binadamu za wahamiaji, katika muktadha wa ushirikiano wao katika kudhibiti uhamiaji.

Mtaalam huyo amesema, anakaribisha mabadiliko muhimu ya kisheria na kitaasisi katika sera za uhamiaji za Uturuki, yakiwemo kuweka sheria mpya kuhusu wageni na ulinzi wa kimataifa, ambayo itaidhinishwa kwenye kikao kijacho cha bunge, na ambayo itaruhusu kutekeleza sheria ya Muungano wa Ulaya kuhusu uhamiaji. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)