Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atilia Shaka Machafuko ya Mali

Ban atilia Shaka Machafuko ya Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Mali na hivyo kukwamisha juhudi za utoaji wa misaada ya usamaria mwema katika upande wa kaskazini mwa taifa hilo.

Ghasia zinazoendelea kuzuka kwenye eneo hilo zimesababisha pia kubomolewa kwa moja ya jengo lenye historia ya pekee katika mji wa Timbuktu.

Ban amezitaka pande zinazozozana kuweka akilini jukumu la kulinda uridhi wa utamaduni wa asili uliopo nchini Mali na amekilaani kitendo cha kushambulia eneo moja la asili.

Mapigano hayo yalizuka tena mwezi January katika upande wa kaskazini mwa taifa hilo baina ya vikosi vya serikali dhidi ya waasi wa kundi la Tuareg wanaotaka kujitenna .