Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yakaribisha mpango wa Muungano wa Ulaya wa kumaliza ulanguzi wa watu

IOM yakaribisha mpango wa Muungano wa Ulaya wa kumaliza ulanguzi wa watu

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekaribisha hatua ya Muungano ya Ulaya ya kuzindua mpango kati ya mwaka 2012na 2016 wa kumaliza tatizo la usafishaji haramu wa watu.

Mpango huo wa miaka mitano unalenga kutambua waathiriwa wa vitendo vya usafirishaji haramu wa watu , kuwafikisha mbele ya sheria wahusika, kuongeza ushirikiano na mashirika mengine katika kupambana na vitendo hivyo.

Tangu mwaka 1994 IOM imekuwa ikifanya jitihada za kupambana na ulanguzi wa watu ambapo imebuni zaidi ya miradi 800 ya kupambana na ulanguzi wa watu kwa zaidi ya nchi 100 kote duniani. Msemaji wa IOM, Jumbe Omari Jumbe ameielezea radio ya UM ni vipi hasa mbinu hii ya Muungano wa Ulaya hufanya kazi.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)