Malaysia yatakiwa kulinda makundi ya kiraia

8 Juni 2012

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa katika maeneo ya uhuru, ameitolea mwito serikali ya Malaysia kuhakikisha inachukua mkondo sahihi kuzilinda taasisi za kiraia ambazo kwa sasa zinapigia upatu kufanyika kwa marekebisho kwa sheria zinazozingatia uchaguzi.

Mtaalamu huyo Ambiga Sreenevasan,amesema kuwa serikali ya Malaysia inapaswa kutoa ulinzi kwa makundi ya kiraia ambayo yapo mstari wa mbele kupigania haki ya kufanyiwa marekebisho kwa mifumo ya uchaguzi.

Ripoti za hivi karibuni zinaonyesha kuwepo kwa hali ya vitisho vinaelekezwa kwa makundi hayo ya kiraia na wakati mwingine vitisho hivyo vimepindukia mipaka.

Ametaka kuheshimiwa kwa uhuru wa kijieleza na kuyaacha makundi hayo ya kiraia yakishiriki vyema kwenye harakati za ujenzi mpya wa taifa hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter