Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna Pillay aizuru Pakistan Juni 4-7

Kamishna Pillay aizuru Pakistan Juni 4-7

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameanza ziara yake ya siku nne nchini Pakistan leo kufuatia mwaliko wa serikali ya nchi hiyo. Ziara hiyo ya siku nne ndiyo yake ya kwanza katika nchi hiyo tangu alipochukua nafasi ya Kamishna Mkuu mwaka 2008.

Wakati wa ziara yake, Mkuu huyo wa haki za Binadamu atakutana na Waziri Mkuu, Yousuf Raza Gilani, Waziri wa Mambo ya Nje, na mawaziri wengine. Pia atafanya mazungumzo na Mkuu wa Sheria, Wabunge, Wanasheria na mashirika ya umma.