Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wenye kuendesha ukatili DRC watafikishwa mbele ya sheria:Pillay

Wenye kuendesha ukatili DRC watafikishwa mbele ya sheria:Pillay

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametoa tahadhari kufuatia kundelea kuongezeka kwa ukatili unaondeshwa na makundi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ukiwemo mauaji, ubakaji, uporaji wa mali na kuchomwa kwa vijiji ambapo ameitaka serikali kuchukua hatua za dharura za kuzuia ukatili huo.

Maafisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC wamekuwa wakichunguza ripoti tangu kuuawa kwa raia na makundi ya waasi kwenye mikoa ya kivu kaskazini, Kivu Kusini na Orientale pamoja na tuhuma za ubakaji kwenye eneo la Masisi lililopo Kivu Kaskazini na Mambasa kwenye wilaya ya Ituri.

Marcia Kran amesoma ujumbe kwa niaba ya Kamishna Mkuu Pillay.