Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wasikitishwa na Matukio ya Quebec:Canada

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wasikitishwa na Matukio ya Quebec:Canada

Wataalam huru wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa mikutano ya amani na uhusiano, pamoja na wa kujieleza, leo wameelezea kusikitishwa kwao kuhusu maandamano ya Quebec tarehe 24 Mai, ambayo yalishuhudia vitendo vya ghasia na kukamatwa kwa hadi waandamanaji 700.

Wataalam hao ambao ni Maina Kiai na Frank La Rue, wametoa wito kwa serikali ya muungano ya Canada na ile ya jimbo la Quebec kuheshimu kikamilifu haki za watu kufanya mikutano ya amani, kujieleza na kutengamana kwa wanafunzi ambao wameathiriwa na sheria mbili mpya. Kwa kipindi cha miezi minne ilopita, wanafunzi wamekuwa wakiandamana katika majimbo ya Montreal na kote Quebec dhidi ya kuongezwa kwa karo ya shule, ambayo wanaona kama ni yenye kuwadhulumu na isiyostahili.

Wataalam hao maalum wamesema kuwa wanawasiliana na serikali ya Canada, ambayo inasema itafafanua mambo haya.