Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel yaanza kuyatafutia Majawabu Malalamiko ya Wafungwa wa Kipalestina

Israel yaanza kuyatafutia Majawabu Malalamiko ya Wafungwa wa Kipalestina

Utawala wa Israel umeanza kuchukua hatua mujarabu kwa ajili ya kutafutia majawabu malalamiko yanayotolewa na wafungwa wa Kipalestina walioko kwenye mikono ya Israel ambao wako kwenye mgomo wa kutokula wakilalamikia kitendo cha kuwekwa kizuizini.

 Wafungwa hao zaidi ya 1,500 wameanzisha mgomo wa kutokula wakiweka shinikizo kwa utawala wa Israel ambao inawashikilia kwenye magereza ya kijeshi na mengine ya siri.

Kulingana na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati Bwana Robert Serry amesema kuwa hata hivyo mgomo ulianzishwa na wafungwa hao ulipatiwa ufumbuzi May 14.

Ameongeza kusema kuwa jumuiya ya kimataifa bado inaendelea kujadiliana na pande zote kwa shabaha ya kuleta utengamao kwa wafungwa hao ambao katika siku za karibuni afya zao zilikuwa majaribuni kutokana na mgomo huo.

 Amesifu hatua zinaanza kuchukuliwa na utawala wa Israel kunusuru maisha ya wafungwa hao.