Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi ni lazima zifanye hima kabla ya mkutano wa Rio+20:Ban

Nchi ni lazima zifanye hima kabla ya mkutano wa Rio+20:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka wawakilishi wa nchi kufanya hima na kuikalisha nyaraka ambayo itatekelezwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu wa mwezi ujao.

Mkutano huo unaofahamika kama Rio+20 utaandaliwa mjini Rio de Janeiro nchini Brazil kati ya tarehe 20 na 22 mwezi Juni mwaka huu. Akiongea mjini New York wakati wa shughuli za mwisho mwisho za kukamishwa kwa nyaraka hiyo Ban amewataka wanao iandaa mkufanya kujitahidi kwa kuwa muda unayoyoma. Zaidi viongozi wa nchi 130 , wakiwemo maelfu ya wabunge , mameya , maafisa wa Umoja wa Mataifa na viongozi wa mashirika ya umma wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.