Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuzuia Utapiamlo kwa Watoto Yemen kupewe Kipaumbele:UNICEF

Kuzuia Utapiamlo kwa Watoto Yemen kupewe Kipaumbele:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limesema kuwa kupiga vita utapiamlo nchini Yemen ni lazima kupewe kipaumbele, kufuatia mkutano wa ‘Marafiki wa Yemen’, ulofanyika Riyadh. Mkutano huo ambao umetambua kuzorota kwa hali ya kibinadamu nchini humo, umeahidi kuchanga hadi dola bilioni 4 za kimarekani ili kukabiliana na hali hiyo. Shirika la UNICEF linasema kuna haja ya dharura ya hatua za haraka ili kuwasaidia watoto milioni 13, ambao wanachangia nusu ya idadi nzima ya watu nchini Yemen. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)