Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la kuwatenga raia wa Roma linaendelea:UNDP

Suala la kuwatenga raia wa Roma linaendelea:UNDP

Raia wengi wa Roma wanaendelea kukabiliwa na ubaguzi na kutengwa kijamii kote barani Ulaya kwa mjibu wa ripoti iliyochapishwa kwa pamoja na Sshirika la muungano wa Ulaya kwa ajili ya haki za msingi FRA na shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo UNDP.

Mashirika hayo mawili yanasema hali Roma kwa wastani ni mbaya kuliko hali ya watu ambao sio Waroma wanaoishi katika maeneo ya jirani. Ripoti hiyo imetokana na tafiti mbili zilizohusu hali ya kiuchumi na kijamii kwa raia wa Roma na wasio Waroma ambao wanaishi katika nchi za jirani 11 za muungano wa Ulaya.