Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka mataifa ya Asia na Pacific kuongeza ushirikiano wa maendeleo:ESCAP

UM wataka mataifa ya Asia na Pacific kuongeza ushirikiano wa maendeleo:ESCAP

Katibu Msimamizi wa Tume ya Uchumi na Kijamii kwa maeneo ya Asia na Pasific, ESCAP, ametoa wito kwa mataifa ya maeneo hayo kushirikiana ili kuendeleza ukuaji wa kiuchumi na mazingira, wakati maeneo hayo yakikabiliwa na uhaba wa rasilmali na kutokuwepo usawa wa kijamii. Dr. Noeleen Heyzer ameyasema haya wakati akihutubia mkutano wa viongozi wa maeneo hayo mjini Bangkok hii leo.

Pia amewahimiza viongozi hao wafanye juhudi ili kukabiliana vilivyo na changamoto zinazojitokeza wakati huu, ili kuongeza maendeleo ambayo sio tu ya namna nyingi, ila pia yawe ya ushirikiano na ambayo ni endelevu.