Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaotenda dhuluma za ngono katika vita waadhibiwe:Wahlstrom

Wanaotenda dhuluma za ngono katika vita waadhibiwe:Wahlstrom

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa maswala ya Dhuluma za ngono katika maeneo ya vita, Bi Margot Wahlstrom, amesema kuwa ni lazima wanaotenda uhalifu wa dhuluma za ngono wakati wa vita waadhibiwe.

Bi Wahlstrom ameyasema haya wakati akihitimisha ziara yake nchini Colombia. Ameongeza kuwa, ingawa anaelewa taifa hilo linataka kutizama mbele badala ya kuzingatia yalopita, hakuwezi kuwepo amani ya kudumu bila amani na usalama kwa wanawake.

Amesema kuwa ni lazima ziongezwe juhudi za kuwasaida waliodhulumiwa ili wapate haki na kuhisi wanakubaliwa katika jamii. Ameongeza kuwa rasilmali zaidi zitahitajika ili kuongeza nguvu za vyombo ya haki na sheria ili viweze kulishughulika suala la ukatili wa ngono.