Mashirika ya Kutoa Misaada yataka Adhabu kwa wahalifu wa ngono wakati wa Vita Colombia

17 Mei 2012

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maswala ya ukatili wa ngono katika maeneo ya vita, Bi Margot Wallstrom, amekutana na mashirika ya umma nchini Colombia kama sehemu ya ziara yake nchini humo. Bi Wallstrom anaizru Colombia ili kupata ufahamu wa moja kwa moja wa tatizo hilo. Mjumbe huyo ameelezea kusikitishwa kwake baada ya kusikiliza ushuhuda wa wanaharakati ambao walielezea visa vingi vya ukatili na dhuluma dhidi ya wanawake, ikiwemo ubakaji, ukatili wa ngono na ukandamizaji.

Mjumbe huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaja kuwa mojawepo ya matatizo makubwa zaidi wanayokumbana nao wanawake ni vitisho kutoka kwa makundi yenye silaha, ili kuwafanya waogope kutafuta haki kwa suala hili.

Ameongeza kuwa wafanyikazi wengi wa umma ambao wana jukumu la kufanya uchunguzi katika uhalifu wa ngono unaohusiana na vita, wanakabiliwa pia na vitisho hivi.

(SAUTI YA MARGOT WAHLSTROM)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter