Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rio+20 ni fursa ya kuiweka dunia katika njia muafaka:Zukang

Rio+20 ni fursa ya kuiweka dunia katika njia muafaka:Zukang

Mkutano wa kimataifa wa Rio+20 ni fursa ya kuiweka dunia katika njia endelevu zaidi ambayo inajumuisha ukuaji wa uchumi unaojali mazingira, usawa wa kijamii na njia bora ya kulinda afya ya dunia kwa muda mrefu amesema Sha Zukang mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya uchumi na jamii.

Katika taarifa yake siku ya Jumatatu kwenye mkutano wa maendeleo endelevu mjini Brisbane Astralia Zukang amesema endapo maandalizi ya Rio+20 yametoa mtazamo wowote basi mtazamo wa msingi ni kwamba ushirikiano wa maendeleo utakuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa maendeleo endelevu.