Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Cambodia yatakiwa kuonyesha uwazi inaposhughulikia masuala ya ardhi

Serikali ya Cambodia yatakiwa kuonyesha uwazi inaposhughulikia masuala ya ardhi

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Cambodia Surya P. Subedi ameitaka serikali ya Cambodia kuonyesha uwazi wakati inaposhughulikia masuala ya kiuchumi na yale yanayohusiana na ardhi.

Subedi ameutaja umuhimu wa hali ya jamii za kiasili ambao uhusiano wao na ardhi unafahamika. Aidha aliipongezaa serikali ya Cambodia kufuata mipangilio ya umiliki wa ardhi kwa jamii za kiasili .

Akiwa kwenye ziara ya siku nane nchini Cambodia Subedi alikutana na maafisa wa utawala wa mikoa , waziri wa mazingira , wizara ya ardhi yakiwemo mashirika kadha yasiyokuwa ya kiserikali.