Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNIDO na KOICA kusaidia tatizo la mazingira Cambodia

UNIDO na KOICA kusaidia tatizo la mazingira Cambodia

Umoja wa Mataifa leo umetangaza kuanza mpango mpya wa mashirikiano na Jamhuri ya Korea kwa ajili ya kuipiga jeki Campodia kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa mazingira.

Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Vienna baina ya shirika la Uamoja wa Mataifa linalohusika na uendelezaji viwanda UNIDO na shirika la maendeleo la Korea KOICA. Koica inatazamia kuipatia UNIDO kiasi cha dola 900,000 ambazo zitatumika kugharimia mradi maalumu wa kukabiliana na tatizo hilo la uchafuzi wa mazingira huko Cambodia.

Kama sehemu ya ufumbuzi wa tatizo hilo, pande hizo mbili zinatazamiwa kuainisha teknolojia mazingira ambayo itasafirishwa hadi Cambodia. Mradi huo pio unatazamia kutupia jicho sekta ya maji ambayo imeharibiwa kutokana na shughuli za viwanda.