Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu akutana na Kofi Annan kujadili Syria:

Rais wa Baraza Kuu akutana na Kofi Annan kujadili Syria:

Rais wa Baraza Kuu Nassir Abdulaziz Al-Nasser leo amekutana na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu, Kofi Annan kujadili mgogoro wa Syria.

Viongozi hao wamejadili hasa jinsi ya kutekeleza mpango wa Bwana Annan wenye hatua sita, kabla yake yeye kutoa ripoti kwa Baraza la Usalama hii leo.

Rais Al-Nasser amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuyashulikia mawswala haya, kwa mujibu wa maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa and Baraza la Usalama, ambayo yanaeleza msimamo wa pamoja dhidi ya mzozo wa Syria.

Rais was Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ameunga mkono juhudi za Bwana Annan, na akatoa wito kwa jamii ya kimataifa kumuunga mkono juhudi hizo.

Rais Al-Nasser amehimiza umuhimu wa serikali ya Syria na wahusika wengine kushirikiana na Bwana Annan na wasaidizi wake, ili kutekeleza kikamilifu maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama, ili kuumaliza mgogoro na kuwawezesha wa-Syria kurejesha amani, utulivu na umoja nchini mwao.