Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM kutathmini sera ya uhamiaji kwenye mipaka ya nchi za Ulaya

Wataalamu wa UM kutathmini sera ya uhamiaji kwenye mipaka ya nchi za Ulaya

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanakusudia kuendesha utafiti wa mwaka mmoja kwa ajili ya kubaini athari zitokanazo na sera za uhamiaji katika eneo la Ulaya na Mediterranian.

 Utafiti huo unatazamiwa kuanza hapo jumatatu ukiangazia zaidi namna nchi za Ulaya zinavyosimamia sera zake za mipakani. Lakini pia utatupia jicho suala linalohusika na haki za binadamu.

 Utafiti huo unakuja katika wakati ambapo nchi nyingi barani Ulaya zikitumia mfumo mpya unaojulikana kama schengen.

 Wataalamu hao wamesema kuwa dhima kubwa ya utafiti huo ni kuangalia mfumo huo mpya unaotumiwa na nchi za Ulaya kama umeleta athari zozote kwenye eneo linalohusika na haki za binadamu.