Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei ya chakula imepungua kidogo lakini ujumla bado iko juu:FAO

Bei ya chakula imepungua kidogo lakini ujumla bado iko juu:FAO

Bei ya chakula duniani kwa mtazamo wa bei wa shirika la chakula na kilimo FAO imeshuka kwa pointi tatu au asilimia 1.4 kuanzia mwezi Machi hadi April mwaka huu, lakini inaonekana kurejea tena katika kiwango cha juu cha pointi 214.

Mtazamo huo wa FAO unasema kushuka kidogo kwa bei hizo ni kwa kwanza baada ya miezi mitatu mfululizo ya ongezeko la bei ya chakula. Hata hivyo FAO inasema licha ya kushuka huko bado kuko juu ikilinganishwa na pointi 200 zilizoshuhdiwa wakati matatizo ya chakula 2008. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)