Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa UM na AU wawasili Chad kujadilia kitisho cha LRA

Maafisa wa UM na AU wawasili Chad kujadilia kitisho cha LRA

Maafisa wa ngazi za juu kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wamewasili nchini Chad kwa ajili ya mkutano wa pamoja wa kuiasa serikali ya nchi hiyo namna inavyokabiliwa na kitisho cha kuandamwa na kundi la Lord Resistance Army.

Kunawasiwasi kwamba, LRA huenda ikaanza kuzipeleka hujuma zake mpya kwa Chad ikiwa ni harakati za waasi hao kupanua katika mataifa mengine baada ya kutuwama kwa miaka mingi nchini Uganda.

Maafisa hao wa kimataifa wanasema kuwa kutokana na mbinyo mkubwa kwa LRA, kuna wasiwasi pengine wakachukua shabaha mpya ya kuhamia katika nchi jirani ya Chad.

Ujumbe huo ukiwa nchini humo unatazamiwa kukutana na rais wa Chad Idriss Déby na baadaye utatoa tahadhari kwa nchi hiyo kuchukua hatua za kujihami na hujuma dhidi ya waasi hao.