Navi Pillay kuzuru Guatemala kutathimini hali ya haki za binadamu

8 Machi 2012

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay atakwenda nchini Guatemala Jumapili wiki hii kujadili na serikali na jumuiya za kijamii  masuala ya haki za binadamu .

Wakati wa ziara yake Bi Pillay atakutana na Rais Otto Perez Molina, makamu wa rais  wa nchi hiyo, waziri wa mambo ya nje, waziri wa ulinzi na viongozi wengine.

Pia atajadili na wabunge, viongozi wa mahakama kuu ya nchi hiyo, wa mahakama ya katiba, mwanasheria mkuu wa serikali na kitengo cha haki za binadamu nchini humo.

Pillay atakutana pia na watetezi wa haki za binadamu, wawakilishi wa jamii za watu wa asili, wajumbe wa jumuiya ya kimataifa, jumuiya za kijamii na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Mada kuu zitakazotawala mikutano yake ni usalama, haki, haki za watu wa asili, ubaguzi, haki za wanawake na hali ya watetezi wa haki za binadamu. Bi Pillay atakuwa Guatemala kwa siku nne.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter