Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa CTBTO akaribisha taarifa za DPRK kusitisha majaribio ya nyuklia

Mkuu wa CTBTO akaribisha taarifa za DPRK kusitisha majaribio ya nyuklia

Katibu Mkuu wa shirika la tume ya maandalizi ya kusitisha majaribio ya nyuklia CTBTO Tibor Toth Alhamisi amekaribisha tangazo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK kwamba imekubali kusitisha majaribio ya nyuklia.

Tobor amesema anakaribisha hatua hiyo ya DPRK na kuongeza kuwa hii ni hatua muafaka inayoelekea kunakostahili. Amesema anatumaini kwamba hatua hii itafungua njia ya baadaye DPRK kutia saini na kuridhia mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia na hilo litasaidia kuingia mapema utekelezaji wa mkataba huo pamoja na nchi saba zilizosalia kuridhia mkataba huo.