Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu la UM akutana na maafisa wa serikali ya Uingereza

Rais wa Baraza Kuu la UM akutana na maafisa wa serikali ya Uingereza

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amefanya mazungumzo na Jeremy Browne ambaye ni mbunge na waziri wa jimbo moja nchini Uingereza.

Wawili hao walizungumzia visiwa vya Falklands/ Malvinas, hali nchini Syria na mpango wa amani wa mashariki ya kati.

 Wote walibadilishana maoni yao kuhusu Somalia hasa mkutano wa juma lililopita kuhusu Somalia ulioandaliwa na serikali ya Uingereza.

 Aidha walizungumzia masuala kuhusu mkutano wa tano wa Umoja wa Mataifa hasa kuhusu masuala ya bajeti ya Umoja wa Mataifa na maandalizi ya huduma za kulinda amani.