Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Urusi imesema haitounga mkono jaribio la kufanya HRC kutoa shinikizo la Kisiasa

Urusi imesema haitounga mkono jaribio la kufanya HRC kutoa shinikizo la Kisiasa

 

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Gennandy Gatilov amesema kwamba Urusi haitounga mkono jaribio lolote la kufanyia mabadiliko baraza la haki za binadamu au HRC kuwa chombo cha kutoa shinikizo la kisiasa na kugawanya mataifa iwe kwa vizuri au vibaya.

Waziri huyo ameongeza kwamba ni muhimu matatizo yaliyopo yakatatuliwa na watu wenyewe husika bila shinikizo na kuingiliwa na nguvu kutoka nje.

Amesema Urusi imekuwa ikipinga ghasia zozote dhidi ya raia lakini pia imekuwa ikipinga matumizi ya silaha kutoka nje kwa kuunga mkono upande mmoja kati ya pande zinazozona katika nchi.

Urusi inashawishika kwamba moja ya changamoto kubwa zinazoikabili jumuiya ya kimataifa leo hii ni kuzuia na kusitisha itikadi kali za kikabila na kidini, kuukomesha ubaguzi wa rangi pamoja na kukabili mauaji ya kibaguzi na kutovumiliana.

(SAUTI YA GRANDY GITLOV)