Zambia yapongezwa kwa kuimarisha demokrasia

27 Februari 2012

Nchi ya Zambia imepongezwa kutokana na kufanya vizuri katika maeneo kadhaa ikiwemo ukuzaji wa demokrasia, ongezeko la wanafunzi wanajiunga na elimu ya msingi na kupunguza kwa vifo vya kina mama wajawazito. Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-moon wakati alipokutana na rais wan nchi hiyo Michael Sata, akihitimisha ziara ya kiserikali nchini humo.

Hii ni ziara ya kwanza kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuitembelea Zambia.

Ban pamoja na mambo mengine pia alitambua mchango mkubwa wa Zambia waliopoteza maisha wakati wakikitumikia kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.

Kwa upande mwingine Ban alilitaka kuheshimiwa kwa haki za msingi kwa makundi ya watu ikiwemo wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja. Amesema kuwa makundi hayo ya watu kama ilivyo watu wengine wanapaswa kutetea vyema na kuheshimiwa kwa haki zao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter