Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani mashambulizo kwenye makao yake nchini Afghanistan

Umoja wa Mataifa walaani mashambulizo kwenye makao yake nchini Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani shambulizi lililotokea kwenye makao yake yaliyo kwenye mji ulio kaskazini mashariki wa Kunduz. Hata hivyo hamna visa vyovyote vya majeruhi vilivyoripotiwa na bado wafanyikazi wote wa Umoja wa Mataifa wako salama.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa ghasia kwenye mji wa Kunduz zinahusiana na kuchomwa kwa nakala za Quran na wanajeshi wa Marekani walio Afghanistan. Watu wanne waliripotiwa kuuawa kwenye ghasia hizo na wengine kujeruhiwa.