Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka amani kufuatia mauwaji ya watu kadhaa nchini Libya

UM wataka amani kufuatia mauwaji ya watu kadhaa nchini Libya

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama nchini Libya, katika wakati ambapo watu saba waliokosa makazi wakiripotiwa kuuwawa.

Mashambulizi hayo yamefanyika katika eneo karibu na kituo cha mafunzo uongozaji meli cha Janzur kilichopo karibu na Tripoli. Watoto watatu na wanawake wawili walipoteza maisha kwenye shambulio hilo wakati wengine wane walivamia na kuuliwa katika mji wa Tawerga.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyofuatilia ulinzi wa amani nchini Libya vimekaribisha hatua ya kurejesha utengamao kwenye maeneo yanayoshuhudia machafuko.

Vikosi hivyo hata hivyo vimeitolewa mwito mamlaka ya dola kuchukua hatua za haraka kuwasaka wahusika wa matukio hayo na kuwafikisha kwenye mkono wa haki.