Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watalamu wa UM kuhusu haki za binadamu wapinga kesi ya Garzon

Watalamu wa UM kuhusu haki za binadamu wapinga kesi ya Garzon

Wataalamu kadhaa huru wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameshutumu kesi dhidi ya jaji mmoja maarufu nchini Hispania kufuatia jitihada zake za kuchunguza zaidi ya madai 100,000 ya kutoweka kwa watu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe chini ya utawala wa Francisco Franco.

Kesi dhidi ya jaji Baltasar Garzon kwa sasa inaendelea nchini Hispania baada ya jaji huyo kuchunguza malalamishi kuhusu uhalifu dhidi ya ubibanadamu. Kesi kama hizo haziruhusiwi kutokana na sheria iliyowekwa baada ya kifo cha Franco. Juma lililopita mahakama nchini Hispania ilikataa ombi la kutaka kufutiliwa mbali kwa kesi dhidi ya Garzon.