Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu la UM akutana na maafisa wa Ufaransa kujadilia maendeleo endelevu

Rais wa Baraza Kuu la UM akutana na maafisa wa Ufaransa kujadilia maendeleo endelevu

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amekuwa na majadiliano na maafisa wa ngazi ya juu ya Ufaransa wakijadilia masuala mbalimbali lakini lile walilolipa uzito zaidi ni juu ya maendeleo endelevu.

Nassir Abdulaziz Al-Nasser amekutana na maafisa wa serikali mjini Paris akiwemo waziri wa mambo ya nje Alain Juppé ambao wote kwa pamoja wametupia macho haja ya kusukama mbele agenda ya maendeleo endelevu.

Viongozi hao wameweka zingatia juu ya mkutano wa kimataifa unaojulikana kama Rio +20 ambao umepangwa kufanyika baadaye mwaka huko huko Brazil.

Mkutano huo unaoratibiwa na Umoja wa Mataifa ni jukuwaa la kimataifa ambalo linaweka shabaha ya maendeleo endelevu ili kuinusuru dunia na mabadiko ya tabia nchi.