Amos asikitikia hali mbaya katika jimbo lililokubwa na mapigano ya kikabila la Jonglei Sudan Kusini

Amos asikitikia hali mbaya katika jimbo lililokubwa na mapigano ya kikabila la Jonglei Sudan Kusini

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura  ambaye amefanya ziara katika jimbo lililokubwa na mapigano ya kikabila la Jonglei huko Sudan Kusini amesema hali katika eneo hilo ni mbaya.’

Katika ziara yake hiyo Bi Valerie Amos, amejionea namna waathirika wa mapigano hayo ya kikabila walivyotuowa mkono na mahitaji muhimu ya kijamii kiasi cha kufanya kuishi katika maisha ya upweke.

Amesema wengi wao wamepoteza ndugu na jamaa zao huku wengine wakipoteza mali na wengine kusababishiwa ulemavu pamoja na kuachwa katika hofu ya maisha.

Amezitaka pande zote zinazojiingiza kwenye mipagano hayo kuweka kando magomvi na ametaka kuanza kutolewa kwa misaada ya dharura kwa waathirika wa machafuko hayo.