Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka Rais wa zamani wa Haiti ashitakiwe kwa ukiukaji wa haki za binadamu

UM wataka Rais wa zamani wa Haiti ashitakiwe kwa ukiukaji wa haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea hofu yake juu ya taarifa kwamba Rais wa zamani wa Haiti Jean Claude Duvalier huenda asishitakiwe kwa ukiukaji wa haki za binadamu uliotekelezwa wakati wa utawala wake kisiwani humo na kwamba anaweza kukabiliwa tuu na makosa ya ufisadi.

Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema kuna nyaraka zinazoelezea kwa kina ukiukaji wa haki za binadamu ukiwemo utesaji, ubakaji na maaji yaliyotokea wakati wa utawala wa bwana Duvalier.

Bi Pillay amesema serikali ya Haiti itakuwa inashindwa kutimiza wajibu wake wa kuwalinda raia wake endapo wahusika wa ukiukaji wa haki za binadamu watafikishwa katika mkono wa sheria. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Jean-Claude Duvalier alikuwa Rais wa Haiti kuanzia mwaka 1971 hadi alipopinduliwa mwaka 1986. Alirejea Haiti Januari mwaka jana baada ya kishi hamishoni nchini Ufaransa kwa miongo miwili.