Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wato bado wanashikiliwa Guantanamo Bay:Pillay

Wato bado wanashikiliwa Guantanamo Bay:Pillay

Mahabusu ya Guantanamo bado iko wazi na inaendelea miaka mitatu baada ya serikali ya Marekani kutoa amri ya kufungwa. Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema amevunjwa moyo kwamba mahabusu huyo bado inatumika, na kwamba washukiwa wanaoshikiliwa katika mahabusu hiyo wanashikiliwa kinyume na sheria za kimataifa.

Pillay amesema serikali zinawajibu na haki ya kuwalinda watu wake dhidi ya vitendo vya kigaidi, pale penye ushahidi dhidi ya wanaoshikiliwa Guantanamo, basi washitakiwe na kuhukumiwa au waachiliwe huru.

Ametaka madai ya utesaji katika mahabusu hiyo yachunguzwe na wahusika wapelekwe kwenye mkono wa sheria. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)