Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa takwimu za uhamiaji kwenda ulaya

IOM yatoa takwimu za uhamiaji kwenda ulaya

Ripoti mpya iliyozinduliwa hii leo na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM mjini Buenos Aires nchini Argentina imeonyesha kuongezeka kwa idadi ya watu kutoka nchini Argentina kwenda nchini Hispania wakati wa miaka kumi ya mwisho wa karne ya ishirini. Ripoti hiyo inasema kuwa Hispania ilikuwa kituo muhimu cha wahamiaji kutoka Afrika, Mashariki mwa Ulaya na Amerika Kusini wakati wa miaka ya tisini.

Takriban wahamiaji 500,000 waliwasili nchini Hispania kila mwaka. Idadi ya wahamiaji kutoka Amerika Kusini iliongezeka kutoka wahamiaji 160,500 mwaka 1990 hadi wahamiaji 708,700 kabla ya kuongezeka hadi wahamiaji milioni 2.1 kati ya mwaka 2001na 2009. Jemin Pandya ni msemaji wa IOM.