Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali na wadau wa afya wakabiliana na kipindupindu DRC

Serikali na wadau wa afya wakabiliana na kipindupindu DRC

Mlipuko wa kipindupindu umeikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hasa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo hususani mjini Bunia wilayani Ituri, pia maeneo ya Koga, Matete na Kesenyi kwenye mtandao wa ziwa Albert.

Kwa mujibu wa duru za afya za serikali maradhi hayo sasa yameingia pia kwenye maeneo ya Kivu ya Kusini mjini Bukavu.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya yakiwemo mashirika ya kimataifa, mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO, na mashirika yasiyo ya kiserikali wanafanya juhudi kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na maradhi hayo, kuyadhibiti na kuchukua tahadhari.

Mwandishi habari wa kujitegemea Mseke Dide amezuru maeneo yaliyoathirika na maradhi hayo na kuandalia makala hii. Ambatana naye.

(MAKALA NA MSEKE DIDE )