Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nishati inahitajika ili kupiga vita umaskini barani Asia na Pacific:UM

Nishati inahitajika ili kupiga vita umaskini barani Asia na Pacific:UM

Utafiti mpya kutoka kwa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kuhusu Asia, na Pacific unatoa wito wa kuwepo nishati ya kisasa itakayotumika kwenye mapishi na umeme ili kutumika kupata mapato na kuboresha afya na elimu.

Ikitolewa juma moja na wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipofanya uzinduzi wa kampeni ya kumhakikishia kila mmoja nishati ripoti hiyo imebaini kuwa hakutakuwa na maendeleo bila nishati na umaskini hautamalizwa bila ya huduma bora za nishati. Flora Nducha na taarifa kamili.

(SAUTI YA FLORA NDUCHA)