Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ya Magharibi kukabiliwa na tisho jipya la usalama

Afrika ya Magharibi kukabiliwa na tisho jipya la usalama

Mashambulizi ya mabomu nchini Nigeria na uwezekano wa hali ya ghasia Guinea-Bissau baada ya kifo cha Rais wa nchi hiyo kunazusha tishio jipya la usalama katika kanda ya Afrika ya Magharibi. Mashambulizi ya bomu ya kundi la Boko Haram hivi karibuni nchini Nigeria yamekatili maisha ya watu wengi. Hofu hiyo ya usalama imeainishwa kwenye ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu shghuli za ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi iliyowasilishwa kwenye Baraza la Usalama Jumatatu.

Said Djinnit ambaye ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu amesema uharamia, uhalifu wa kupangwa na usafirishaji wa mihadarati pia vinachangia kuliweka eneo zima la Afrika ya Magharibi katika mtafaruku. Wakati huohuo ripoti imeelezea maendeleo mazuru yaliyojitokeza kama kufanyika kwa uchaguzi katika baadhi ya nchi za ukanda huo.