Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Slovakia yachaguliwa kuongoza ECOSOC

Slovakia yachaguliwa kuongoza ECOSOC

Mwanadiplomasia kutoka nchini Slovakia amechaguliwa kuongoza Baraza la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya uchumi na jamii ECOSOC, ikiwa ni miongoni mwa chombo muhimu ndani ya Umoja huo wa Mataifa.

 Miloš Koterec kabla ya kuchaguliwa kwake, alikuwa akishikilia nafasi ya makamu wa rais kwenye chombo hicho.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kwake, Milos ametaja vipaumbele vyake ikiwemo pia kuanzisha mipango mipya itayosaidia kutanzua mambo wakati kunapojitokeza hali ya sintofahamu kwenye uchumi wa dunia.

 Amesema kuwa jukumu lake kuu atalolitilia kipaumbele ni pamoja na kubadilisha hali ya mtizamo wa dunia kuhusiana na maendeleo na kuhaidi kuanzisha njia mpya ambayo itakuza mashirikiano baina ya nchi wahisani na zile zinazopokea misaada.